Articles on political party manifestos coming soon in IsiZulu and English. Yazi ngaphambi kokuba uvote!
Iliyoandikwa na Pheliswa Msele
Kiswahili: iliyoandikwa na Esther Johnson
Iliyochapishwa Aprili 9, 2026
Kwa karne nyingi, vyanzo vikubwa vya maji vimechukuliwa kama maeneo matakatifu na jamii kadhaa za Kiafrika. Kuanzia kuwa vyanzo vya uponyaji hadi kuwa viunganishi muhimu na ulimwengu wa kihoro, maji yametumika kwa mengi zaidi ya kukata kiu tu.
Je, ni vipi basi, maeneo ambayo yameaminika kuwa na nguvu na uhusiano mkubwa kiasi hicho, yamegeuzwa kuwa mapipa ya taka na majalala? Je, inaweza kuwa ni mabadiliko ya binadamu kuwa kizazi kisicho na imani za kishirikina, na hivyo kutojali maji, au inaweza kuwa ni kukua kwa sekta ya biashara na umaarufu wa vyakula vya kubeba (takeaways) na plastiki? Au, je, ni ukosefu tu wa elimu juu ya umuhimu wa bahari na umuhimu wa kutupa vizuri vitu vya plastiki? Ni jambo la heri kwamba kuna vitabu vya watoto ambavyo vinazungumzia masuala haya. Kitabu cha watoto cha Zandile Ndhlovu kiitwacho Wimbo wa Zandi (Zandi's song), kinafundisha na kuangazia uchafuzi wa plastiki kwa njia rahisi lakini yenye fikra kwa watoto.
Katika kitabu hicho, Zandi, mhusika mkuu, anaelezwa na bahari kuhusu historia ya uhusiano kati ya jamii na viumbe wa baharini, na jinsi uhusiano huo ulivyofika kikomo kwa sababu ya wakoloni na uchafuzi wa maji. Bahari inaendelea kumwambia Zandi kwamba atakaporundi nyumbani, lazima awajulishe watu wake juu ya umuhimu wa kuyaweka maji safi. Mwandishi, ambaye pia ni mwalimu wa kwanza mwanamke mweusi wa kupiga mbizi bila mitungi ya oksijeni nchini Afrika Kusini (freediving), anaendelea kupigania utunzaji wa mazingira katika harakati zake. Kauli yake nzito aliyoitoa katika mjadala, ambayo ni ukweli rahisi ambao wengi wanapaswa kuufahamu, ni jinsi "Lengo la Maendelo Endelevu (SDG) 14 inavyosalia kuwa lengo lenye ufadhili mdogo zaidi." Kwa male ambao huenda hawajui, SDG 14, kulingana na Umoja wa Mataifa nchini Afrika Kusini, inahusu maisha yaliyo chini ya maji. Maisha ya chini ya maji yina yanajumuisha viumbe wanaojulikana kama pomboo, mwani, na kamba-maji, hadi viumbe wasiojulikana na mafumbo yanayosubiri kugunduliwa. Uchafuzi wa maji unatishia viumbe hawa na kusababisha uharibifu wao na hatimaye kutoweka kabisa. Viwanda mbalimbali vikiwemo vya matibabu, magari, chakula na vinywaji, na biashara za rejareja hutumia plastiki katika shughuli zao.
Plastiki za kutumika mara moja tu ndizo zinazochangia zaidi uchafuzi wa plastiki. Shirika kubwa la haki za mazingira, Greenpeace, linaitaja mahususi kampuni ya Coca-Cola kama mchangiaji mkubwa zaidi wa uchafuzi wa plastiki. Makala ya Ocean inasema, "Utafiti uliofanyiwa mapitio na wataalamu katika jarida la Science uligundua kuwa Coca-Cola ndiye mchafuzi namba moja wa plastiki zenye chapa zilizopatikana kwenye mazingira."
Plastiki hizi zinajumuisha zadi vijidudu vya plastiki (microplastics) ambavyo hutokana na vitu kama chupa na vifuniko vya chupa, miongoni mwa vingine. Sasa, kwa nini ni muhimu tulinde maji wakati tunaishi nchi kavu? Je, umakini wetu haupaswi kuelekezwa zaidi kwenye ardhi kuliko baharini? Kweli, bahari na maji hutumikia kusudi kubwa zaidi kuliko kukata kiu tu. Bahari ni makao ya viumbe mbalimbali wa baharini ambao hutumikia kama chakula kwa manadamu. Samaki, kamba, kamba miti, na wengine wengi huishi baharini. Maisha ya mwanadamu yanabaki hatarini mradi tu maisha ya baharini yawe hatarini.
Bahari ni mchangiaji mkubwa wa oksijeni kwani mimea mingi ya baharini hushiriki katika usanisinuru (photosynthesis). Vijidudu vya plastiki huchangia katika upungufu wa oksijeni (deoxygenation) baharini. Kulingana na Kamusi ya Collins, upungufu wa oksijeni hurejelea mchakato wa kuondoa oksijeni kutoka kwenye kitu, kama vile maji au hewa. Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa katika Nature ulionyesha kuwa ulaji wa vijidudu wadogo wa baharini (zooplankton) unaweza kuharakisha upotevu wa oksijeni baharini. Hii hutokea kwa sababu viumbe hawa wanapokula vijidudu hivyo, wanaweza kula kiasi kidogo cha chakula chao cha asili, jambo ambalo linaweza kuathiri uzalishaji wa viumbe hai vinavyozama na kutumia oksijeni vinapooza kwenye kina kirefu cha bahari.
Uchafuzi wa plastiki una madhara mbalimbali hasi, ikiwa ni pamoja na nyanja za kiikolojia na kijamii na kiuchumi. Makala ya jarida la Heliyon ya mwaka 2020 inaeleza kwa ufupi kwamba uchafuzi wa plastiki baharini una athari mbaya za kiikolojia, ikiwa ni pamoja na kunaswa, ulaji wa sumu, kukosa hewa, na kuvurugika kwa maisha ya baharini. Pia hubadilisha mifumo ya kiekolojia na kusababisha upotevu wa bayoanuwai (Biodiversity) na huduma muhimu.
Aidha , athari hizi huenea hadi kwenye nyanja za kijamii na kiuchumi zinazoathiri viwanda kama vile utalii na uvuvi, pamoja na afya ya binadamu, na hatimaye kutishia ustawi wa mazingira na jamii za wanadamu. Kwa hivyo, uchafuzi wa plastiki hauishii tu kwa wanyama wa baharini kufa, bali unaenena hadi kwenye maisha ya mwanadamu kwa njia nyingi.
Ni mikakati gani tunaweza kuteleza ili kupunguza idadi ya plastiki zinazoishia baharini na vyanzo vingine vya maji, zikitishia si tu maisha ya baharini, bali pia maisha yetu kama wanadamu? Kususia bidhaa kumethibikita kufanya kazi katika matukio fulani, lakini wakati chapaa kubwa ambazo zimejenga misingi imara na uhusiano wa kihisia na watumiaji, na zinaweza kumudu kupoteza mamilioni ya dola kwa wiki chache, ndizo zinazolengwa, kuna matumaini kidogo kuwa hatua hiyo itatosha. Bila kusahau kutotabirika kwa matumiaji wenyewe katika utamaduni ambapo ni rahisi kuchukua hatua siku chache za kwanza za hamasa, lakini wakati sababu inapopoteza kasi polepole, kila kitu kinarudi kama kilivyokuwa awali, ikiwa ni pamoja na mazoea ya watumiaji.
Mipango, sera, sheria n.k., zina jukumu muhimu katika ulinzi wa bahari dhidi ya vichafuzi hatari. Mashirika makubwa na madogo ya haki za mazingira, wanaharakati wa mazingira, pamoja na serikali wanapaswa kufanya kazi pamoja katika mapambano ya kuwa na bahari salama, yenye afya, na safi zaidi. Elimu juu ya umuhimu wa bahari, maisha ya baharini, na vyanzo vya maji kwa ujumla, inapaswa kutolewa kwa kiwango kikubwa. Hii ni pamoja na elimu na uhamasishaji wa plastiki zinazoweza kutumika tena au vifungashio vilivyotengenezwa kwa njia endelevu. Upatikanaji wa plastiki hizo unapaswa kuenea kote ili iwe rahisi kwa watumiaji kuzipata.
Hebu wazia ulimwengu usio na pomboo, mwani, kasa, papa, au uzuri wa kuvutia wa bahari. Si taswira nzuri, au siyo? Ndiyo maana sote unapaswa kutimiza wajibu wetu katika kulinda maji yetu.