Articles on political party manifestos coming soon in IsiZulu and English. Yazi ngaphambi kokuba uvote!
Esther Johnson
Siku hizi vijana wengi hutumia muda mwingi kwenye simu, mitandao ya kijamii na video fupi. Lakini kusoma vitabu bado ni jambo muhimu sana kwa maisha yetu. Vitabu hutusaidia kujua mambo mapya na kutafakari zaidi kuliko tunavyofanya tukitazama video tu.
Vitabu vilivyoandikwa na Waafrika vina tusaidia kuelewa maisha ya kila siku tunayoyaishi. Tunaposoma hadithi za Kiafrika, tunaona lugha, mila na shida ambazo tunazifahamu. Hii hutufanya tujione kwamba maisha yetu pia yana maana na yanastahili kusimuliwa. Kusoma pia kunasaidia kuboresha lugha yetu ya kuandika na kuongea. Kadiri tunavyosoma maneno na sentensi nyingi, ndivyo tunavyojua kuandika vizuri insha, barua na makala. Hili linaweza kutusaidia shuleni na hata katika kazi baadaye.
Mwisho, kusoma vitabu hutufungulia ndoto mpya. Tunaposoma kuhusu watu waliopambana wakafanikiwa, tunapata moyo was kuamini kwamba hata sisi tunaweza kufika mbali. Ngiyo maana ni muhimu vijana tujipe muda, hata dakika ishirini kila siku, kusoma kitabu chochote tulicho nacho nyumbani au maktaba.