Articles on political party manifestos coming soon in IsiZulu and English. Yazi ngaphambi kokuba uvote!
Ngano ya Kenya
Hadithi ya Luanda Magere ni moja kati ya hadithi zinazosimuliwa katika kabila la Waluo nchini Kenya. Ingawa kuna matoleo mengi, kiini cha hadithi kinabaki kuwa kilekile: mtu aliyekuwa hashindiki. Baadhi ya watu wanaamini kuwa hadithi hii ndiyo sababu ya ndoa kati ya Waluo na Wakipsigis kuwa adimu sana nchini Kenya.
Luanda, au Lwanda Magere, alizaliwa mwaka wa 1720 kwa wazazi Abonyo Wuod Omolo na Nyabera. Mama yake alifariki wakati wa kujifungua, hivyo Luanda alilelewa na nyanga yake, Rapondi. Luanda alikopuwa akianza tu umri wa ujana, baba yake aliuawa katika moja ya vita kati ya Waluo na maadui wao wa jadi, Wanandi.
Luanda alikua na kuwa mwanamume mwenye nguvu kiasi kwamba wazee wa Kiluo walimwamini kuwamaliza wapinzani wao vitani. Alipigana kwa ustadi mkubwa, akiwaua maadui zake bila juhudi nyingi. Hii ni kwa sababu Luanda hakuwa kama watu wengine. Alikuwa na nguvu zisizo za kawaida. Mwili wake uliumbwa kwa mwamba, si nyama. Mikuki na marungu vilitua mwilingi mwake na kudunda badala ya kutoboa ngozi yake, hali iliyomfanya asishindike vitani. Hata Wanandi walijitahidi vipi, hakuna kitu kilichoweza kumdhuru Luanda. Badala yake, wao ndio waliojikuta wakitoroka kila walipoona wapiganaji wao wengi wametandazwa chini, wakiwa wameuawa na Waluo kwa msaada wa Luanda.
Wanandi, wakiwa wamechoka kushindwa na Waluo, waliketi na wazee wao na kubuni mpango wa kumuua Luanda. Waliamua kumpa mooja wa wanawake wao ili amuoe, wakisingizia kuwa ni toleo la amani. Sababu halisi ya kumpa Luanda. mke ilikuwa ni ili mwanamke huyo agundue udhaifu wa Luanda, kisha Wanandi wamuue. Waluo walimshauri Luanda asimwoe mwanamke huyo, lakini hakusikiliza ushauri wao, jambo ambalo lilifanikisha mpango wa Wanandi.
Kwa muda mrefu, mwanamke huyo wa Kinandi alingoja kwa uvumilivu dalili ya udhaifu kutoka lwa mumewe, lakini hakuna kilichotokea. Kisha siku moja, Luanda aliugua. Mke wake wa kwanza ambaye kwa kawaida alimwuguza alikuwa hayupo, akimwacha Luanda na yule mke wa Kinandi pekee. Luanda alimwagiza mke wake akate kiluvi chake na kupaka dawa. Mke alifanya kama alivyoambiwa na alishtuka kuona kikivuja damu. Usiku huo, alitoroka nyumbani kwa Luanda na kukimbia kwa matu wake wa Kinandi kuwaambia alichogundua. Ukweli uliokuwa umesababisha vifo vya wanajeshi wengi wa Kinandi na kushindwa mara nyingi uliwekwa wazi. Chanzo cha nguvu na kutoshindwa kwa Luanda kilikuwa kwenye kivuli chake.
Wapiganaji wa Kinandi walishambulia Waluo kwa nguvu. Waluo walipigana kiume, huku Luanda akiwaua wapiganaji wengi wa Kinandi. Kwa bahati mbaya kwa Waluo, Wanandi walikuwa na silaha moja ambayo ingekuwa maangamizi kwa Waluo: maarifa. Mmoja wa wapiganaji wa Kinandi alirusha mkuki uliokwenda moja kwa moja kwenye kivuli cha Luanda, naye akaanguka, ameshindwa. Wakati wapiganaji wa Kiluo wakilia kwa hofu na Luanda akitoa maneno yake ya mwisho; lanaa kwa ndoa kati ya Mluo na yeyote kutoka makabila ya Kipsigis. Mwili wake uligeuka kuwa jiwe polepole, jiwe ambalo lingebaki kuwa sehemu muhimu ya historia milele.
Mpaka leo, ni watu wachache sana wanaothubutu kuvunja laana ya Luanda. Mahali ambapo mawe yake yamebaki pamekuwa eneo la kihistoria nchini Kenya. Muhimu zaidi, hadithi yake imepitishwa kutoka kizazi hadi kizazi kama simulizi la tahadhari.
Kama hadithi nyingi za kale, hadithi ya Luanda Magere ina matoleo mengi. Majina "Nandi" na "Lang'o" wakati mwingine hutumiwa kwa kubadilishana katika ngano hii. Katika moja ya matoleo, Luanda hakuugua, balu alitoa siri yake akiwa amelewa huku mke wake akisikiliza.
Marejeleo:
Luanda Magere. Wikipedia, Wikimedia Foundation, 7 June 2024.
Nzuki, P., Traditional tales, journals.co.za/doi/abs/10.10520/AJA02578301_20